Taarifa ya Faragha
Faragha yako ni muhimu sana kwetu. Katika Taarifa hii ya Faragha (Taarifa ya Faragha) tumeeleza namna Shirika la Stichting Justdiggit (Justdiggit au sisi) linavyotumia taarifa zako binafsi ambazo hukusanywa kupitia Aplikesheni yetu ya Kijani (Aplikesheni ya Kijani).
Tumejizatiti kulinda faragha yako na kuhakikisha usalama wa taarifa zako binafsi. Tafadhali soma Taarifa hii ya Faragha kwa makini ili uelewe namna tunavyozitumia taarifa zako binafsi na jinsi tunavyozishughulikia.
Nani anadhibiti taarifa?
Taarifa zako binafsi zinakusanywa na Justdiggit. Ofisi yetu iliyosajiliwa iko Prins Hendrikkade 25, 1012 TM Amsterdam. Unaweza kuwasiliana nasi kwa njia ya baruapepe info@justdiggit.org au kwa simu +31 (0) 20 737 23 66. Vilevile, Aplikesheni ya Kijani inakuwezesha kuwasiliana nasi kwa njia ya WhatsApp. Sisi ni wadhibiti wa taarifa chini ya Sheria Majumui za Ulinzi wa Taarifa (GDPR), tunashughulika na kuamua namna na sababu za kutumika kwa taarifa zako binafsi.
Tunakusanyaje taarifa zako binafsi?
Taarifa zako binafsi (a) hutolewa na wewe mwenyewe; na (b) sisi huziandaa kutokana na maelezo yako wakati wa mazungumzo yetu na wewe.
Aina ya taarifa binafsi tunazozikusanya kwa matumizi yetu pamoja na msingi wa kisheria unaotumika katika uchakataji wetu wa taarifa.
Katika muktadha wa matumizi yako ya Aplikesheni ya Kijani, tunakusanya, tunahifadhi, na tunatumia taarifa zako binafsi kwa mpangilio kama ilivyo katika kipengele cha ‘taarifa binafsi’ hapa chini. Pia, hapa chini utaona lengo la uchakataji na msingi wa kisheria tunaoutumia kwa kila aina ya taarifa binafsi tunayoichakata kuhusu wewe.
Kama utashindwa kutoa taarifa fulani inayokuhusu wewe unapoombwa, tunaweza kushindwa kutekeleza wajibu wetu wa kisheria na matakwa ya kimkataba au tutashindwa kufanya shughuli fulani.
Ni muhimu sisi kuwa na taarifa zako binafsi zilizo sahihi na zilizosasishwa. Tafadhali, tujulishe ikiwa taarifa zako binafsi zitabadirika wakati unapoendelea kutumia Aplikesheni ya Kijani.
Je, taarifa zako binafsi tunazihifadhi kwa muda gani?
Hatuchakati taarifa zako binafsi kwa muda mrefu kuliko inavyohitajika kulingana na madhumuni ya uchakataji.
Katika muktadha huu tunahifadhi taarifa zako binafsi kwa muda mrefu kadiri ya uhai wa akaunti yako katika Aplikesheni ya Kijani. Taarifa zako binafsi zitafutwa miaka mitano baadaye, tangu akaunti yako ilipotumika kwa mara ya mwisho katika Aplikesheni ya Kijani, au zitafutwa moja kwa moja baada ya wewe kufuta akaunti yako katika Aplikesheni ya Kijani.
Ikiwa tuko chini ya kipindi maalumu cha kisheria cha uhifadhi wa taarifa, tutahifadhi taarifa zako binafsi kwa muda uliowekwa kisheria.
Hata hivyo, tunaweza kuhifadhi taarifa zako binafsi kwa muda mrefu zaidi kwa ajili ya madai ambayo yanaweza kuletwa dhidi yetu hapo baadaye.
Wakati mwingine, tunaweza kuficha utambulisho wa taarifa zako binafsi ili zisihusiane na wewe tena, katika mazingira hayo tunaweza kutumia taarifa hizo pasipo kukujulisha.
Je, taarifa zako binafsi tunazitumia na nani?
Ikiwa hii ni muhimu katika Aplikesheni ya Kijani, tutawapa taarifa zako watoa huduma wengine kwa maelekezo na chini ya uangalizi wa Justdiggit. Watoa huduma hao wanachukuliwa kama “wachakataji” chini ya GDPR. Katika mazingira hayo, taarifa zako binafsi zitabaki chini ya udhibiti wa Justdiggit. Watoa huduma hao wakati wote watazingatia maelekezo ya kimaandishi ya Justdiggit, ikiwa ni pamoja na wajibu wa kiusalama. Taarifa zako tunazitumia na wachakataji walio katika makundi yafuatayo:
Pia, tunaweza kutoa au kusambaza taarifa zako binafsi:
- katika makundi yetu kwa madhumuni ya kibiashara, kama vile kiutawala, kiusimamizi na madhumuni ya kiuhasibu, na ikiwa ni sehemu ya shughuli za kawaida za utoaji wa ripoti za utendaji kazi wa kampuni, katika muktadha wa kuboresha biashara au zoezi la urekebishaji wa kundi, kwa ajili ya kusaidia matengenezo ya mfumo na utunzaji wa taarifa;
- kama tunauza kampuni letu au sehemu yake (ikiwa ni pamoja na mali tofauti), au kama tutaungana na kampuni nyingine. Katika mazingira hayo, tunaweza kutumia taarifa zako na mmiliki mpya au yeyote tuliyeungana naye, lakini ni kwa kiasi ambacho kinahitajika kulingana na madhumuni ya uchakataji wa taarifa zako binafsi;
- ikiwa tutakabiliwa na kesi za ufilisi, kama sehemu ya uuzaji wa mali zetu na mfilisi (au anayefanana naye); au
- tunalazimika au tunaruhusiwa kisheria kufanya hivyo. Katika mazingira kama hayo, tutaipa taarifa zako binafsi mamlaka husika ya usimamizi au chombo kingine cha serikali.
Je, taarifa zako binafsi tunazihifadhi wapi?
Justdiggit inahifadhi taarifa zako binafsi katika kanzidata zilizopo ndani ya Eneo la Kiuchumi la Ulaya (EEA).
Haki zako
Kwa mujibu wa sheria zinazotumika katika Umoja wa Ulaya, una haki ya kupata, haki ya kurekebisha, haki ya kufuta, haki ya kuzuia uchakataji, haki ya kuhamisha pamoja na haki ya kupinga. Kumbuka kwamba, haki nyingi zilizotajwa hapa si kamilifu na ziko chini ya misamaha ya kisheria, na zinaweza kutumika kwa aina fulani tu ya taarifa binafsi au uchakataji.
Hapa tunaeleza kwa undani zaidi kuhusu haki zako na kutoa taarifa binafsi namna unavyoweza kutumia haki zako.
Tutajibu ombi lako ndani ya mwezi mmoja, lakini tuna haki ya kuongeza muda huo mpaka miezi miwili. Kama tutaongeza kipindi cha majibu, tutakujulisha ndani ya mwezi mmoja kuanzia ulipotuma maombi.
- Kupata: una haki ya kutuuliza kama tunachakata taarifa zako binafsi na, ikiwa tunachakata, unaweza kuomba kuzipata taarifa zako (kwa kawaida hujulikana kama “ombi la kupata taarifa”). Hii inakuwezesha kupata nakala ya taarifa zako binafsi tulizonazo na kuhakikisha kwamba tunazichakata kisheria. Kama itadhihirika kuwa ombi lako halina msingi au limezidi, tunahifadhi haki ya kutoza ada inayofaa au kukataa kutekeleza katika muktadha huo.
- Kusahihisha au kusasisha: una haki ya kuomba na kuhakikisha kwamba taarifa yoyote binafsi isiyo kamili au isiyo sahihi tuliyonayo kuhusu wewe ni sahihi.
- Kufuta: katika muktadha fulani, una haki ya kutuomba tufute au tuondoe taarifa zako binafsi. Hata hivyo, tunaweza kukataa ombi lako la kufuta kulingana na mazingira, kwa mfano, wakati ambapo taarifa zako binafsi zinahitajika kwa mujibu wa sheria au kuhusiana na madai. Wakati tunapohitaji kutegemea msamaha, tutakujulisha.
- Kuzuia: una haki ya kutuomba kusitisha uchakataji wa taarifa fulani miongoni mwa taarifa zako binafsi, kwa mfano, ikiwa unataka tuzingatie usahihi wake au tutoe sababu ya kuichakata.
- Kuhamisha: unaweza kuomba uhamisho wa nakala ya taarifa zako binafsi kwenda kwa mshirika mwingine (kama inawezekana kitaalamu). Una haki ya kutuomba tutoe taarifa zako binafsi katika mtindo unaosomeka kwa urahisi kwa kampuni nyingine. Kumbuka kwamba, haki hii inatumika katika taarifa binafsi ulizotupa na ikiwa tutatumia taarifa zako binafsi kwa msingi wa idhini au ambapo tulitumia taarifa zako binafsi kuingia mkataba na wewe.
- Kuzuia/Kupinga: wakati tunachakata taarifa zako binafsi kulingana na maslahi halali, utaweza kupinga uchakataji kufanyika. Vilevile, una haki ya kupinga wakati tunachakata taarifa zako binafsi kwa lengo la kupata maelezo mafupi. Ingawa, tunaweza kuwa na haki ya kuendelea na uchakataji wa taarifa zako binafsi kwa msingi wa maslahi yetu halali.
- Kuondoa idhini yako: wakati ambapo umetoa idhini ya kuturuhusu kuchakata taarifa zako binafsi, pia unaweza kuondoa idhini hiyo wakati wowote. Ikiwa utaondoa idhini hiyo, bado haitaathiri uhalali wa tuliyoyafanya kwa kutumia taarifa zako binafsi kabla ya kuondoa idhini husika.
Kama unataka kutumia mojawapo ya haki hizi, au kuondoa idhini yako, tafadhali wasiliana nasi kwa maandishi kupitia baruapepe info@justdigit.org.
Haki ya kuwasilisha malalamiko
Pia, una haki ya kuwasilisha malalamiko katika mamlaka ya usimamizi, hususan katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ambapo wewe ni raia wake, ambapo unafanya kazi au mahali ambapo madai ya ukiukaji wa sheria ya ulinzi wa taarifa yamewasilishwa. Orodha ya mamlaka za usimamizi zilizopo katika Umoja wa Ulaya pamoja na mawasiliano yake, vinapatikana hapa.
Nchini Uholanzi, unaweza kuwasilisha malalamiko katika Autoriteit Persoonsgegevens (simu. +31 70 888 8500 au kupitia https://autoriteitpersoonsgegevens.nl/en).
Mabadiliko ya taarifa ya faragha
Taarifa hii ya faragha itabadilishwa kulingana na wakati.
Tunaweza kubadilisha taarifa hii ya faragha kadiri muda unavyoenda. Wakati wote, tutachapisha toleo lililosasishwa katika Aplikesheni ya Kijani. Ikiwa tutafanya mabadiliko yoyote muhimu katika taarifa hii ya faragha (mfano, kuhusu taarifa binafsi tunazozikusanya, namna tunavyozitumia au kwa nini tunazitumia), tutakujulisha.