sw
App Namba 1 katika Ukijanishaji

Boresha shamba lako

Play Store QR code Swahili
Skani ili upakue
Udongo wenye afya
Mavuno yanaongezeka
Maisha bora

Habari, rafiki yangu! Ninafurahi kuwa nawe hapa. Kwa kutumia App ya Kijani, unajifunza kuhusu mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuifanya ardhi yako kuwa ya kijani na yenye rutuba.

Udongo wenye afya

Mbinu za ukijanishaji utakazojifunza katika app hii zitakusaidia kutunza maji katika ardhi yako na kuzuia mmomonyoko wa udongo. Ukitunza ardhi yako utaufanya udongo uwe na afya na rutuba.

Mavuno yanaongezeka

Udongo wenye rutuba hutunza virutubisho ambavyo hutumika kama chakula cha mazao yako, nyasi na miti hustawi vizuri.

Maisha bora

Kwa kuboresha ardhi yako, unaboresha na mazingira yako pia. Unatengeneza sehemu ya kijani na yenye hewa nzuri kwa kuishi.

Ninaitwa Baraka, na kwa kushirikiana na wakufunzi wenzangu, tunafurahi sana kukufundisha jinsi ya kuboresha ardhi yako! Huu ni utangulizi tu wa yale utakayokutana nayo baada ya kupakua app ya Kijani. Pakua app hii sasa ili ufurahie faida zake!

Ninaitwa Baraka, na kwa kushirikiana na wakufunzi wenzangu, tunafurahi sana kukufundisha jinsi ya kuboresha ardhi yako! Huu ni utangulizi tu wa yale utakayokutana nayo baada ya kupakua app ya Kijani. Pakua app hii sasa ili ufurahie faida zake!

Habari mpya

Watu zaidi ya 1,200 wapakua Kijani App

Familia yetu inazidi kuongezeka! Ikiwa ni wiki chache tu tangu uzinduzi rasmi kufanyika Tanzania, tayari Kijani App imepakuliwa zaidi ya mara elfu moja. Kama mmoja wa watumiaji wetu alivyotueleza hivi karibuni: Kijani ni ya Tanzania, na Afrika Mashariki yote! Tunadhamiria kueneza Kijani App kwa watu wengi zaidi.

Uzinduzi wa Kijani App Tanzania!

Tunafurahi kutangaza kuwa, Kijani App imezinduliwa rasmi Tanzania katika maadhimisho ya Nanenane. Kwa pamoja na Washirika wetu, Justdiggit imeshiriki maonesho ya Arusha, Mbeya na Dodoma ambapo Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde alizindua App. Wakitoa maoni kuhusu Kijani App, Wakulima wametoa pongezi, na kusema wamefurahishwa na Ubunifu huu.

Uzinduzi wa App ya Kijani Siku ya Nanenane

App ya Kijani itazinduliwa rasmi katika siku muhimu sana: Siku ya Nanenane! Shirika la Justdiggit, LEAD Foundation na washirika wengine, kwa furaha kubwa tutaijuza dunia kuhusu app ya Kijani. Tuna hamu kubwa sana kusherehekea mchango mkubwa wa wakulima na wafugaji pamoja na wewe.

Hapa chini utaona maswali yaliyoulizwa mara nyingi zaidi. Bofya alama ya ▽ ili kusoma jibu.

Tembelea Justdiggit

App hii ni kwa ajili ya wakulima wadogowadogo na wafugaji wanaotaka kujifunza na kufanyia mazoezi mbinu za ukijanishaji ambazo ni rahisi kuzitekeleza zitakazowasaidia kuboresha ardhi zao na kuongeza mavuno yao na/au malisho ya mifugo.

Mbinu za ukijanishaji unazoweza kujifunza katika app hii ni zile zinazofaa katika usimamizi mzuri wa ardhi. Katika sehemu ya “Maarifa”, utakutana na mada kuhusu mbinu za ukijanishaji zenye masomo ya kinadharia, maswali na jinsi ya kuzitumia katika ardhi yako. Baadhi ya mada unazoweza kuzitarajia ni pamoja na:

  • Utangulizi wa app ya Kijani
  • Kisiki hai
  • Mashimo ya zai
  • Kuweka matandazo
  • Kontua na miteremko
  • Fanya juu na fanya chini
  • Vizuizi vya nyasi
  • Kutengeneza mboji
  • Matuta ya kuvunia maji
  • Kilimo mseto
  • Uzalishaji wa chakula cha mifugo

Baadhi ya masomo haya bado yapo katika maandalizi, lakini yatawekwa hivi karibuni. Pia, tutakuwa tukiongeza masomo mengine zaidi yatakayowasaidia wafugaji.

Mada zote zinafundishwa na wakulima wetu mahiri na wenye uzoefu, ambao wataeleza kila hatua na watakufundisha mbinu na kila unachotakiwa kujua ili nawe uanze. Mbinu hizi zote zimethibitishwa, ni mbinu zenye mafanikio, na nyingi zimeanzishwa Afrika na Waafrika.

Isipokuwa suala la kutumia kidogo intaneti yako kupakua app na masomo, unaweza kutumia vifaa vyako kujifunzia mbinu hizi. Mtu yeyote anaweza kufanya jambo hili!

 

Shirika la Justdiggit linarudisha uoto wa asili katika mazingira yaliyoathirika barani Afrika kwa kutumia mbinu mbalimbali za kukijanisha, pia kupitia vyombo vya habari na teknolojia ya simu.

Washirika wetu wana ujuzi na elimu ya kutosha katika utunzaji wa mazingira. Pamoja, tunarudisha uoto wa asili kwenye maeneo yaliyoharibika barani Afrika. Hii inaleta athari chanya kwa mazingira na jamii.

Ikiwa wewe ni shirika linalotamani kushirikiana na Justdiggit, tafadhali tutumie ujumbe katika baruapepe info@justdiggit.org. Je, umeshawahi kusikia kuhusu Greener.LAND tool? Tovuti hii imeundwa ili kusaidia mashirika ya kilimo kuamua kuhusu mbinu ipi ni nzuri zaidi katika miradi ya uboreshaji wa ardhi. 

Kama wewe ni mkulima au mfugaji na ungependa kuuliza maswali au kutoa maoni yako kuhusu app ya Kijani, tafadhali tutumie ujumbe kwa njia ya WhatsApp kwenye namba +255 760 327 450 au piga simu +255 762 116 460.

Tembelea tovuti ya Justdiggit kama unataka kujua zaidi kuhusu app ya Kijani au miradi mingine ya ukijanishaji.

Tembelea Justdiggit