sw

Taarifa ya faragha

Imesasishwa: [Desemba 8] 2023

Habari na karibu kwenye Kijani! Aplikesheni hii imetengenezwa kwa upendo wa Shirika la Justdiggit la Uholanzi (ofisi iliyosajiliwa ipo Prins Hendrikkade 25, 1012 TM Amsterdam, namba ya usajili: 51457008). Kijani ipo hapa kukupa vidokezo na ushauri juu ya kuifanya ardhi yako kuwa ya kijani zaidi na kilimo chako kuwa bora zaidi.

Kukubaliana na Masharti Yetu

Unapotengeneza akaunti na/au unapotumia Kijani, ina maana kuwa unakubaliana na sheria na ahadi zilizomo katika Vigezo na Masharti na Taarifa yetu ya Faragha. Kama hukubaliani, basi tuwie radhi, kwani utalazimika kuacha kutumia aplikesheni hii.

Kipengele cha  Vigezo na Masharti kinajumuisha makubaliano ya kisheria kati yako na Shirika la Justdiggit juu ya matumizi yako ya aplikesheni.

Mambo Yanapobadilika

Kuna wakati tunaweza kubadilisha Vigezo na Masharti haya. Kama tukibadili, tutakujulisha mapema, isipokuwa sheria ikitutaka tufanye tofauti. Kama utaendelea kutumia Kijani baada ya mabadiliko kuwekwa, ina maana kuwa unakubaliana nayo na utazingatia sheria mpya. Ikiwa haukubaliani na sheria hizi au Vigezo vyovyote vya matumizi vilivyosasishwa, unaweza kufuta akaunti yako.

Faragha na Ulinzi wa Taarifa

Faragha yako ni muhimu sana kwetu. Aplikesheni yetu, Kijani, huomba baadhi ya taarifa kutoka kwako ili kufanya ushauri tunaoutoa uwe bora na kufanya uone yote ni kwa ajili yako. Kwa mfano, tunaweza kukuuliza unalimia wapi, ardhi yako ikoje, na aina ya mazao unayolima. Kumbuka, taarifa hizi unatupatia kwa hiari yako, na tunaahidi kuzitunza wakati wote. Tutazitumia taarifa hizi kwa ajili ya kusaidia kuboresha ushauri tunaokupa na hatutaziuza kwa yeyote. Namna yetu ya kushughulikia taarifa zako inazingatia kanuni kali kutoka katika sheria inayoitwa GDPR. Kama unataka kujua zaidi kuhusu jinsi tunavyolinda na tunavyotumia taarifa zako, tafadhali tazama katika Taarifa yetu ya Faragha. 

Kutengeneza Akaunti Yako

Unaweza kutengeneza akaunti yako ya Kijani kwa kutumia jina utakalolichagua na pengine unaweza kuweka na picha pia, kama unapenda. Hakikisha kwamba unatunza taarifa za akaunti yako na usimpe mtu yeyote azitumie kwa sababu wewe ndiye unayesimamia akaunti yako.

Matumizi na Utumiaji Mzuri

Jisikie huru kutumia mambo mazuri yote kwenye Kijani na uwashirikishe na wengine kwa kuzingatia Vigezo na Masharti haya. Hakikisha unawajulisha mahali ulipoipata hii. Kuna baadhi ya vitu unavyoviona hapa vinaweza kuwa ni vya watu wengine na vinaweza kuwa vinalindwa na hakimiliki na sheria nyingine, kwa hiyo, tafadhali heshimu vitu vyao pia. Huruhusiwi kutumia sehemu yoyote ya maudhui katika aplikesheni yetu kwa matumizi ya kibiashara bila kupata idhini ya kufanya hivyo kutoka kwetu au kwa watoa leseni wetu.

Kijani ni sehemu rafiki, kwa hiyo kuna baadhi ya vitu* hatuwezi kuvikubali. Hii  ina maana kuwa hatutaki ujeuri/kutojali hisia, mambo yanayoumiza wengine, na kwa hakika mambo yasiyowapendeza wengi hayahitajiki, kama vile mambo ya kiutu uzima au chuki. Hebu tuifanye aplikesheni yetu iwe safi na njema.

*mambo haya ni pamoja na, kama ilivyoamuriwa na Justdiggit katika mwelekeo wake wa kipekee, kwamba hupaswi:

i) Kuondoa hakimiliki yoyote, alama ya kibiashara, au taarifa nyingine za umiliki kutoka katika sehemu yoyote ya huduma; (ii) Kuzalisha upya, kurekebisha, kuandaa kazi zinazotokana na msingi huu, kugawa, kurasimisha, kukodisha, kuuza, kuuza kwa mara nyingine, kuhamisha, kuonyesha hadharani, kufanya maonyesho hadharani, kusambaza, kuirusha mtandaoni, kutangaza au vinginevyo, kutumia huduma isipokuwa kama sisi tukiruhusu; (iii) Kutenganisha, kuitengeneza upya au kutenganisha huduma isipokuwa kama inavyoweza kuruhusiwa na sheria inayotumika. (iv) Kuunganisha, kufananisha au kuunda sehemu yoyote ya huduma; (v) Kusababisha au kuanzisha programu zozote au maandishi kwa lengo la kuunganisha, kutengeneza faharasa, kuchunguza, au vinginevyo, uchukuaji wa taarifa katika sehemu yoyote ya huduma au kutuelemea kupita kiasi au kukwamisha uendeshaji na/au utendaji kazi wa kipengele chochote cha huduma; (vi) Kufanya chochote kinyume cha sheria, kupotosha, au kulaghai au kwa kutokufuata sheria au dhumuni lisiloidhinishwa; (vii) Kuvunja (au kusaidia au kuhamasisha wengine kuvunja) Vigezo na Masharti haya au sera zetu nyingine. (viii) Kufanya chochote kwa njia ya kukashfu, chuki, jeuri, uchafu, ponografia, kinyume cha sheria au matumizi ya nguvu; au (ix) Kujaribu kupata huduma bila kuidhinishwa, kudhoofisha kipengele chochote cha huduma au mifumo inayohusiana au mitandao.

Haki Unazotupa

Kwa kutumia Kijani, unatupa kibali cha kutumia taarifa zako ulizoziwasilisha ili kuboresha zaidi aplikesheni. Lakini, usihofu, wakati wote tutaheshimu faragha yako.

Nani Anamiliki Nini

Kama unavyojua, mambo yote yanayoifanya Kijani iwe kama ilivyo, kama vile ubunifu, maneno na namna inavyofanya kazi, sisi ndiyo wamiliki. Na ikiwa tunatumia kitu kilichotengenezwa na mtu mwingine, basi watakuwa wameturuhusu tuvitumie.

Si Vigezo na Masharti haya, wala matumizi yako ya Kijani, yanamaanisha au yanakupa haki zozote katika, au zinazohusiana na Kijani, isipokuwa kwa haki ndogo ya mtumiaji iliyotolewa hapo juu.

Tunapoagana

Ikiwa kuna jambo linaenda vibaya kabisa na tunatakiwa kukuzuia kuendelea kutumia Kijani, tutafanya hivyo. Lakini, tunaamini kuwa hatutafikia tatua hiyo. Na kama wewe au sisi tutataka kuachana, baadhi ya sheria hizi bado zitaendelea kutumika.

Tuna haki ya kusitisha akaunti yoyote, wakati wowote, ikiwa kwa utashi wetu tutaona kwamba umeshindwa kutimiza matakwa ya Vigezo na Masharti haya au kama kuna hatari ya kuumizwa au hasara kwa mtu yeyote.

Hakuna Ahadi

Tumeijenga Kijani kuwa msaada kadiri inavyowezekana, lakini hatuwezi kutoa ahadi zozote kwamba wakati wote tutakuwa wakamilifu. Hatutoi dhamana kwamba Kijani itafanya kazi wakati wote pasipo usumbufu, kuchelewa, au hakutakuwa na mapungufu. Tunaitoa aplikesheni ‘kama ilivyo’, ikiwa na maana kwamba hatutawajibika kama kuna kitu hakitakuwa sawa au hakifanyi kazi kama ulivyotarajia.

Si Kosa Letu

Tupo hapa kukupa ushauri na kukusaidia kujifunza, lakini hatuwezi kulaumiwa kama mambo hayaendi kama ilivyopangwa kwa upande wako. Sheria inasema kwamba hatutawajibika kwa vitu kama kupata hasara au kama haujafurahishwa na aplikesheni.

Kwa maneno mengine, hatuhitaji kuwajibishwa kwa: (i) hasara zisizosababishwa na sisi kuvunja Vigezo na Masharti haya au pengine kwa matendo yetu; (ii) hasara ambazo wewe na sisi hatuwezi kuzitabiri, wakati ambao unakubaliana na Vigezo na Masharti haya; (iii) maudhui yoyote yanayoumiza, yasiyosahihi, machafu, yanayovunja sheria, au maudhui yanayopingwa ambayo yamewekwa na wengine unayoweza kukutana nayo kwenye Kijani; na (iv) matukio yaliyo nje ya udhibiti wetu.

Hatutengi au kuzuia kwa namna yoyote wajibu wetu kwako ambapo itakuwa kinyume na sheria kufanya hivyo. Hii ni pamoja na kuwajibika kwa kifo au mtu kuumia kwa sababu ya uzembe au kuvunja haki za mtumiaji.

Kuondoa, kuzuia au kusitisha akaunti yako kama kuna jambo litajitokeza

Kama kuna jambo litajitokeza kwa sababu umetumia Kijani kwa namna ambayo hukupaswa kufanya hivyo (kwa mfano, kama umevunja Vigezo na Masharti haya kwa uwazi kabisa, kwa kukusudia au kwa kujirudiarudia; kama mara kadhaa umekiuka hakimiliki za watu wengine; au ambapo tunatakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria), na linatuletea matatizo, haraka sana, tunaweza: (i) kuondoa maudhui yoyote au taarifa zako zilizomo katika Kijani; na/au (ii) kukataa kukupa au kuacha kukupa huduma zote au sehemu ya huduma (pamoja na kusitisha au kufungia akaunti yako).

Tunafuata Sheria za Wapi

Tunafuata sheria za Uholanzi, mahali tulipo. Kwa hiyo, kama kutatokea hali ya kutoelewana (ingawa hatutarajii), tutatumia sheria za Uholanzi na tutaenda kwenye mahakama iliyopo Amsterdam, Uholanzi, kusuluhisha, isipokuwa kama imeainishwa vinginevyo na sheria za Uholanzi au za kimataifa.

Makubaliano Yetu Kamili

Tulichokiweka hapa ni makubaliano na maelewano yote kati yako na sisi kuhusu matumizi yako ya Kijani. Hii ni picha kamili. Ikiwa kwa sababu yoyote ile, sehemu ya Vigezo na Masharti haya hayatumiki au ikaonekana hazitekelezeki, usihofu, sehemu nyingine zote bado zitaendelea kufanya kazi.

Una Swali?

Je, una maswali yoyote kuhusu Vigezo na Masharti haya? Usisite kutuuliza kupitia info@justdiggit.org.

Kwa kutumia Kijani, inamaanisha kwamba umeshasoma haya yote, unayaelewa, na unakubaliana nayo. Asante kwa kuwa sehemu ya jamii yetu ya kijani!